Tuesday, August 25, 2009

Unawahi kufika kileleni? Unachelewa kupata nguvu za kurudia tendo? Dawa ni hii!

Uwanja wetu wa leo, utakuwa na kazi moja tu, kujadili tatizo la kuwahi kufika kileleni, kuchelewa kupata nguvu za kurudia tendo, chanzo na tiba yake. Dhumuni la kuandika mada hii limetokana na maoni ya wasomaji wengi.

Wasomaji hao ambao wengi ni wanaume, waliniomba niwaandikie hivyo ili kunusuru uhusiano wao. Wengine wapo kwenye ndoa, kwahiyo waliniambia kuwa ushauri wangu unaweza kuwa tiba timilifu kwao.

Hivyo basi, kutokana na kutambua umuhimu wao, ndiyo maana sijasita kuandika haya unayoyasoma.

Tatizo la kuwahi kufika kileleni, mara nyingi huendana na mambo mengine ambayo huchagiza wenzi wengi kusalitiana ama kutengana kabisa.

Wanawake wengi wanagombana na watu wao kwa sababu kama hizi, hawavutiwi kuwaona waume wao wakiwahi kufika kileleni, hivyo kushindwa kuwapa dozi inayotosheleza.

Wanasikitishwa na hali ya wenzi wao ya kukosa nguvu za kutosha wakati wa kufanya tendo la ndoa ama ugoigoi wa kuchelewa kurudiwa na nguvu za kufanya kweli.

Aidha, wanakosa amani wanapobaini kwamba wapenzi wao hawana msisimko wakati wa kufanya yale ‘mambo yetu’. Hata hivyo, tunapogeuka kisaikolojia hili si tatizo kubwa, bali linahitaji kutuliza akili.

Ninaposema kutuliza akili, nakuwa namaanisha kuwa wengi hawana magonjwa yanayohitaji dawa, isipokuwa wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia tu.

Vijana na baadhi ya watu wazima wengine wanaenda kwa waganga na wakati mwingine wakijikuta wanajiingiza katika matumizi ya mitishamba bila kuelewa kwamba ugonjwa wao haupo kwenye kasoro za kimaumbile, bali upo akilini.

Hapa nataka tukubaliane kwamba jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wanaodai kuwa hawana nguvu ni ukosefu wa elimu ya mabadiliko ya kibinadamu na ufahamu duni wa mbinu za kuwawezesha kucheza michezo ya kimapenzi kwa ufanisi.

Mpenzi ni sanaa pana, ina mafunzo mengi na ili uimudu, unatakiwa ujifunze kila siku mabadiliko yaliyopo. Sambamba na hilo, kujua mapito, mazingira, mabadiliko ya mwili na kuyakubali ni mambo ya msingi.

Pamoja na matatizo haya kuwakera wanawake kama nilivyotangulia kusema, huwafanya wanaume kukosa amani. Mara nyingi wanaopata dosari hizi, hujihisi wana nuksi.

Hata hivyo, mshangao unaokuja hapa ni kwamba wanaume hupenda kutafuta mbinu za kutatua tatizo lao bila kuwashirikisha wenzi wao, kana kwamba wao haliwahusu.

Saikolojia inatambua kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni zao la udhaifu wa mke na mume na sio la mwanaume peke yake kama watu wengi wanavyodhani.

Kwa mfano, mwanaume atapata wapi msisimko wa kimahaba kama mwanamke hatakuwa mtundu wa kubuni mbinu za kuufanya mwili uliopoa usisimke?
Atavutiwa nini mwanaume kurudia awamu ya pili, ikiwa kwenye mzunguko wa kwanza alikutana na harufu isiyofaa? Nakshi nakshi humuongezea mwanaume hamu ya kutaka tena na tena. Huo ndiyo ukweli!
Napenda niweke ukweli kweupe, mara nyingi tatizo la msisimko wa kurudia tendo, husababishwa na mwanamke mwenyewe. Kwa maana hiyo, ili litatuliwe ni lazima ziwepo juhudi za pande mbili.

Tuweke kituo kwa leo, nakuomba tukutane wakati ujao ili tuendelee na mada hii. Bila shaka, tutakapokutana ‘ishu’ ijayo, utaweza kung’amua mengi kuhusu somo hili. Mimi na wewe tupo together as one.

1 comments: