Thursday, August 20, 2009

TATAIZO LA NGUVU ZA KIUME

Tafiti mbalimbali duniani zinabainisha kunaongezeko kubwa la watu wanaosumbuliwa na tatizo la nguvu za kijinsia (ED au Erectile dysfunction).

Ingawa tatizo hili huwakumba pia wanawake, wenye kuathirika na kuaibika zaidi ni wanaume, kiasi kwamba baadhi hufikia maamuzi mabaya kwa mfano kujiua nk.

Kulingana na taarifa za shirika liitwalo the National Ambulatory Medical Care Survey (NAMCS), nchini Marekani kati ya wanaume 1,000, watu 22 husumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume/kijinsia hasa wale wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea juu.

Aidha kutokana na kukithiri kwa tatizo hilo, NAMCS inasema zaidi ya watu 2.6 milioni wanatumia dawa za kuongeza nguvu za kiume. Hali ni mbaya pia nchini, hii ndio sababu kuna matangazo mengi ya waganga wa jadi wenye kutibu nguvu za kijinsia, kiasi kwamba inakuwa vigumu kufahamu yupi mkweli yupi mwongo.

Utafiti pia unaonyesha kuwa asilimia 5 ya wanaume wenye umri wa 40 na kuendelea wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo, aidha kati ya asilimia 15 na 25 na wanaume wenye umri wa miaka 65 wanakabiliwa na tatizo hili.

Nimewahi kuandika vitabu kadhaa, kwa mfano kile kiitwacho ?Saikolojia na Utafiti? ambacho nilizungumzia mbinu za kupona tatizo la nguvu za kiume baada ya kushirikiana na watafiti mbalimbali duniani. Ninachotaka uelewe ni kwamba tatizo hili linatibika, cha msingi ni kujua nini cha kufanya, sio kukata tamaa kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya.

Msingi wa kuwa na maisha yenye amani ni kusaka tiba ya kile kinachokusumbua, sio kulia tu.

Tatizo huanzaje?; Umbile la mume lina sehemu (chambers) mbili muhimu ziitwazo corpora cavernosa, na corpora cavernosa.

Aidha kuna sehemu nyingine inaitwa The spongy tissue ambayo inajumuisha misuli na mishipa ya damu. Mwanzo wa tatizo hilo huanzia kwenye ubongo na kitendo cha mwanaume kushindwa kuwa imara ni dalili ya magonjwa mabaya hasa ya moyo, figo nk.

Hisia zinazoingia kwenye ubongo huamka misuli inayopeleka hisia hizo kwenye umbo la mume. Ndio kusema kwamba kutosisimka ipasavyo kwa mume ni dalili kwamba mfumo wa damu hausukumi vizuri.

Kinachofanyika ni kwamba baada ya msisimko, damu hujaa kwenye eneo liitwalo corpora cavernosa, hapo ndipo mwanaume husisimka na kuwa mwenye nguvu.

Wenye magonjwa kama vile kisukari, figo, wenye kuendeleza vileo, kutokula vizuri, kuvuta sigara, kuacha kufanya mazoezi na kujichua wana uwezekano wa asilimia 70 kupata tatizo la nguvu za kijinsia. Takribani asilimia 35 na 50 ya wanaume wenye ugonjwa kisukari, wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume.

Wengine walio katika hatari ya kupata tatizo hili ni wale wenye uzito wa kupita kiasi. Wengine kati ya asilimia 10 na 20 wanasumbuliwa na tatizo hili kwa sababu ya matatizo ya kisaikolojia, kwa mfano kama mwenzi wako alikufanyia jambo baya nk.

Tatizo hili kama nilivyoeleza ni kubwa, hadi ilifikia hatua Mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi, Janet Bina Kahama, 10 Aprili 2007 katika kikao cha saba cha bunge aliuliza swali ambalo lilikuwa namba 8 lenye kipengele a, b, na c ambapo kwenye kipengele b aliuliza: Je, serikali inafahamu ni sababu gani zinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume kunakotangazwa sana na waganga wa jadi?

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Homeli Mwakyusa alijibu kuwa, upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi, baadhi yao ni lishe duni hasa mboga za majani, kutokula aina mbalimbali za jamii ya karanga (nuts), matumizi yasiyofaa ya ulevi kama pombe.

Alisema sababu nyingine kuwa ni matumizi ya sigara na dawa za kulevya, dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya akili na vilevile kutopumzika kunakosababishwa na shughuli nyingi za kijamii hivyo kusababisha uchovu.

Lakini ni kweli dawa hizi za asili zinauwezo wa kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Pro. Mwakyusa anathibitisha kwa kusema kuwa, dawa nyingi za tiba asili ni virutubisho ambavyo muhitaji angeweza kuvipata endapo angekula vyakula vyenye virutubisho hivyo. Pia haijawahi kuripotiwa mtu kuathirika baada ya kutumia dawa hizi.

Ninachotaka kusisitiza katika makala haya ni kwamba ikiwa una tatizo la nguvu za kijinsia, jambo la msingi ni kuangalia staili za maisha unayoishi hasa kwa kuachana na tabia zinazosababisha mtu kupata tatizo hili kama vile ulevi, kuacha kujichua, kujifunza namna ya kuishi na watu tofauti wakiwemo wale wanaokera nk.

Zaidi ya yote unapaswa kujua aina ya vyakula ambavyo ukila vinaweza kukuondolea tatizo hilo. Kwa kawaida kuna vyakula vya aina tofauti, kwa mfamo vya wagonjwa, watoto, watu wa ndoa nk.

Zaidi ya vitu vingine unavyopaswa kuvitumia, unatakiwa kwanza mwenye kutoa tiba kujua udogo au ukubwa wa tatizo. Kumbuka chakula ni chakula, lakini chakula ni tiba, ukitaka kuamini hili, kama una mafua chukua kitunguu swaumu, kiponde jipake chini ya unyayo utapona. Ndio nasema kwamba katika maisha tafuta mbinu za kuondokana na shida inayokukabili kwa njia ya amani, sio kujiua, atafute hufanikiwa, wala usichoke kuhangaika hadi upate unachotaka.

1 comments:

  1. Mimi nakisukari uume wangu mara nyingi unasinyaa baada ya kufanya tendo la ndoa nitumie dawa gani?

    ReplyDelete